A. UTANGULIZI
Tunamshukuru Mungu kwa kutulinda salama hadi leo.Kama mnavyokumbuka ,tulifunga shule tarehe 17 Machi 2020 ,kutokana na mlipuko wa janga la korona COVID 19.
Katika kipindi hiki cha likizo, shule ilitoa kazi tatu za nyumbani kwa watoto ( Holiday package 1 na Holiday package 2). Baada ya tamko la Waziri Mkuu tarehe 17 Aprili 2020, kuwa wanafunzi wataendelea kuwapo nyumbani ilibidi tuongeze kazi za watoto kwa njia ya Whatsapp.Sio wazazi wote waliposajili watoto walituachia namba za Watsapp ,hivyo tulizitumia namba za watsapp tulizokuwa nazo, ambapo robo tatu ya wanafunzi wote walizipata kazi hizi.
Mwanafunzi atapaswa kuwasilisha kazi zote tukifungua shule, yaani holiday package i, Holiday package ii, na zile za watsapp ambazo alizifanya na mzazi ulizisahihisha. Wanafunzi wote ambao hawakupata mazoezi yaliyotumwa kwa watsapp ,watayapata katika website ya shule ,maswali pamoja na majibu.
Tunatanguliza shukrani zetu kwa wazazi kwa kusimamia ufanyikaji wa mazoezi haya ,tunajua haikuwa kazi rahisi kwa watoto kutumia njia za tehama kujifunza ila ilisaidia marudio na kuboresha taaluma.
B.TAREHE MUHIMU ZA MASOMO.
Shule itafunguliwa tarehe 29/06/2020.Wanafunzi watakuwa na likizo fupi ya wiki moja tarehe 28/08/2020 hadi tarehe 06/09/2020. Shule itafungwa tarehe 18/12/2020.
Darasa la saba watakuwa na mtihani wa taifa tarehe 7 na 8 Oktoba 2020
Darasa la nne watakuwa na mtihani wa taifa tarehe 25-26/11 /2020.
Wanafunzi wanaweza kuwa na siku ya mapumziko vipindi vya mitihani ya Mock darasa la saba na la nne na siku za mitihani ya taifa.
- MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA.
- Masomo yatakuwa yanaanza mapema saa 1.00 kamili asubuhi.Ni vyema mzazi ukimuandaa mtoto mapema.
- Mtoto anatakiwa kuwa na barakoa za kitambaa 4, ili aweze kuzitumia awapo shuleni.**Watoto wenye umri chini ya miaka 5 na wenye pumu, hawataruhusiwa kuvaa barakoa**.
Tutajitahidi barakoa hizi zipatikane katika duka la shule,ili ziwe sare.Mzazi utaweka alama katika barakoa ya mtoto,ili iwerahisi kudhibiti wasibadilishane.Mtoto anapokuja Jumatatu, awe nabarakoa yake toka nyumbani.
- Shule imeandaa maji safi na sabuni kwa ajili ya kunawa mikono. hairuhusiwi wanafunzi kutumia sanitizer
- Mwanafunzi akiwa na dalili za ugonjwa wowote, tunakuomba mzazi,usimruhusu kuja shule.Dalili hizi za magonjwa zina fanana ,hivyo akija inaweza ikaleta tafsiri tofauti.Mwanafunzi akija kuripoti baada ya kupona,aje na nakala ya cheti cha matibabu.
**Mtoto akiugua awapo shuleni, tutakutaarifu mzazi.Ikiwa ni ‘serious’ sana ,tutampeleka hospitali ya Palestina.*
**Tunaomba wazazi mu –‘update’ namba za simu ,mtupatie namba ambayo,ina whatsapp na inayopatikana muda wote.****
- Mzazi au mgeni yeyote atakayefika shuleni ili kupata huduma katika ofisi zetu, atanawa mikono getini,au atatumia sanitizer yake mbele ya mhudumu wetu.Atapaswa kuwa umevaa barakaoa ,atapimwa joto ,ndipo ataruhusiwa kuingia ndani ya shule.
- Ni muhimu mzazi kukamilisha malipo ya ada mapema ili kuepuka kukatiza masomo ya mtoto.Akaunti yetu ni 01J1013387200 CRDB Bank – Grace Primary School au unaweza kulipa kwa kutumia Tigo pesa .Namba ya kampuni ni 919293.
- Namba muhimu za simu .
- Mwalimu Mkuu – 0715136851, (0784 136851-Whatsapp) Email: uronuw@gmail.com
- Mwalimu wa Taaluma. 0693364014, (0754824500 – Whatsapp 0766782294 ; 0787929256 ; 0786557964.
- Afisa Usafiri: 0716 904408, 0782904408.
- Mwl wa darasa la Saba, 0715834481 ; 0686522123
- Mwl wa darasa la Nne: Lily 0713741720; Rose 0743566178
- Mwl wa darasa la Sita: Lily 0767061385; Rose 0762 418906
- Mwl wa darasa la Tano: Lily 0715533136; Rose 0688904343
- Mwl wa darasa la Tatu: Lily 0754699461; Rose. 0656177162; Peace, 0743389678. Mwl wa darasa la Pili: Lily: 0658180717; Rose 0755915344; Peace : 0715540422
- Mwl wa darasa la Kwanza: Lily 0782467562; Rose :0713539446; Peace: 0658166665
Asante.
Tunamwamini Mungu aliyetulinda kipindi chote cha mlipuko wa ugonjwa, kuwa atatulinda hata kipindi hiki wanafunzi wakirejea.